Luis
Figo amesema "soka limepotea" baada ya Sepp Blatter kuchaguliwa tena
kuwa rais wa Fifa jana na kumtaka kwa mara nyingine tena kuondoka katika
nafasi hiyo.
Blatter
(79) alimshinda mpinzani wake Prince Ali kutoka nchini Jordan, ambapo
sasa atakaa tena madrakani kwa miaka minne mingine huku akiwa amekaa
madarakani kwa takribani vipindi 5.
Blatter alipata kura 133 dhidi ya 73 za Prince Ali kabla ya mpinzani wake huyo kuamua kujitoa katika raundi ya pili.
Ushindi
wake umekuja huku viongozi 14 wa shirikisho hilo wakiwa wamekamatwa kwa
tuhumu za rushwa siku chache tu kabla ya uchaguzi.
Figo
- ambaye hapo awali alipanga kuwania nafasi hiyo kabla ya kujitoa kwa
madai ya kutozigawa kura ili kurahisisha kumng'oa Blatter, amesema kuwa
amehuzunishwa sana na matokeo ya uchaguzi huo.
"Leo
ilikuwa ni siku nyngine ya giza hapa Zurich," alisema nguli huyo wa
Ureno. "Fifa imepotea, lakini juu ya yote hayo, soka limepotea na kila
mpenda soka amepotea pia.
"Blatter
alitoa sababu za kijinga sana pale aliposema hawezi kudhibiti kila mtu
ndani ya shirikisho. Hilo ni kama tusi kwa wapenda soka. Hawa watu,
ambao Blatter amekuwa akiwatunuku vyeo kwa miaka kadhaa, leo anawageuka,
Fifa sio shirikisho lenye maadili tena.
"Kama
Blatter alihusika kwa udogo katika soka, basi sidhani kama
angechaguliwa. Kama ana upungufu wa maadili, basi ndani ya miaka
michache ijayo atajiuzulu."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni