STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 31 Mei 2015

WAKALA WA ARTURO VIDAL AONEKANA LONDON, AMEFATANINI? TENA ALIKUWA ANAANGALIA FAINALI YA FA

Gazeti la michezo la kila siku la Italia,  Dello Sport, leo jumapili limeripoti kwamba kiungo wa Juventus, Arturo Vidal anahusishwa kujiunga na ligi kuu England.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Arsenal na Manchester United  zinaongoza kuwania saini ya Mchile huyo.
Sehemu ya stori hiyo inasema kwamba wakala wa Vidal, Fernando Felicevich alikuwepo jana kwenye mechi ya fainali ya kombe la FA kati ya Arsenal na Aston Villa.
Hata hivyo, uwepo wa Felicevich katika mechi hiyo ya fainali haushangazi kwasababu pia ni wakala wa mchezaji wa Arsenal, Alexis Sanchez.
Dello Sport  wanasema siku chache zijazo, Felicevich anatarajia kufanya mazungumzo na Arsenal pamoja na Man United ili kuona ni timu gani inaweza kutoa ofa nzuri.
Taarifa kutoka Italia zinaeleza kuwa Juve tayari wameshaanza harakati za kutafuta mbadala wa Vidal ambapo malengo yao makubwa ni kumnasa nyota wa Chelsea,  Oscar,  majira haya ya kiangazi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox