STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 25 Juni 2015

ADRIANO MGUU NDANI MGUU NJE BARCELONA.

WAKALA wa mshambuliaji nyota wa Barcelona, Adriano amedai kuwa mteja wake huyo anaweza kuondoka katika klabu hiyo kutokana na kukosa namba katika kikosi cha kwanza. 

Adriano mwenye umri wa miaka 30 amecheza mechi 16 pekee msimu uliopita akiwa ameanza katika kikosi cha kwanza mechi 10 kati ya hizo. 

Toka Jordi Alba atue Barcelona Adriano amekuwa akipata muda mchache wa kucheza katika kikosi timu hiyo. 

Wakala wa mchezaji huyo Paulo Affonso Neves amesema Adriano amekuwa akifanya kazi kwa bidii lakini hapewi nafasi ya kutosha ya kucheza ndio maana anataka kuondoka kutafuta timu itakayoweza kumpa nafasi hiyo. 

Neves aliendelea kudai kuwa kama Adriano ataendelea kubakia chaguo la tatu Barcelona itakuwa vyema kutafuta mahali pengine lakini hawna haraka katika hilo. Beki huyo wa zamani wa Sevilla ana mkataba na Barcelona unaomalizika mwaka 2017.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox