STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 2 Juni 2015

BERBATOV ATEMWA NA AS MONACO

 

BERBATOV ATEMWA NA AS MONACO

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Bulgaria, Dimitar Berbatov anatafuta timu ya tatu ya kujiunga nayo England, baada ya kutemwa na AS Monaco ya Ufaransa.
 
Berbatov alijiunga na vigogo hao wa Ligue 1 Januari mwaka 2014 kutoka Fulham ya England na atakumbukwa kwa kufunga bao la pili katika ushindi wa 3-1 kwenye dhidi ya Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu.
 
Pamoja na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa yuko huru baada ya kuachwa na Monaco, iliyomaliza katkka nafasi ya tatu kwenye Ligue 1 msimu huu.
 
Katika taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo, Makamu wa Rais wa Monaco, Vadim Vasilyev, amesema; "Dimitar Berbatov ameonyesha kipaji chake chote na soka babu kubwa. Dhahiri ni miongoni mwa washambuliaji wakubwa waliojiunga na AS Monaco. 
 
Tunajivunia alicholeta katika klabu na tunamtakia kila la heri aendako,".'
Berbatov alikuwa na wakati mzuri akichezea klabu ya Tottenham Hotspur kabla ya kujiunga na Manchester United  iliyomsaini kwa dau la Pauni Milioni 30.75 mwaka 2008.
 
Amefunga mabao 48 katika Ligi Kuu ya England katika misimu minne chini ya kocha Sir Alex Ferguson, kabla ya kuhamia Fulham, ambako alicheza kwa msimu mmoja na nusu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox