STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 22 Juni 2015

CECH ATUA ARSENAL

Arsenal imekamilisha usajili wa golikipa wa Chelsea Petr Cech na anatarajiwa kukipiga na klabu yake ya zamani akiwa ametinga uzi wa Emirates kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa Agosti 2 mwaka huu kwenye uwanja wa Wimbley
Cech amesajiliwa kwa dau la pauni milioni 11 baada ya majadiliano marefu kati ya Arsenal na Chelsea juu ya kumsajili Cech yalioanza tangu msimu ulipomalizika na hatimaye wakafikia makubaliano na kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 akasaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Arsenal ukiwa ni usajili wa kwanza kufanywa na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.
Jose Mourinho alikuwa hataki kumuuza Cech kwenda kwa wapinzani wake wa jiji moja la London (Arsenal) japokuwa taarifa hizo hazikuwa na uhakika  wowote.
Awali Paris Saint-Germain iliipelekea ofa Chelsea kwa ajili ya kumsajili mkongwe huyo wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Czech, lakini Cech alisema yeye anapenda zaidi kuendelea kukipiga kwenye vilabu vya jijini London ambapo ndipo ilipo familia yake.
Kutua kwa Cech kwenye kikosi cha Arsenal kunafungua mlango wa kutokea kwa moja ya golikipa wa kikosi hicho kati ya Wojciech Szczesny au David Ospina ambaye amekuwa akifukuziwa na klabu ya Fenerbahce na yeye amekuwa akitaka kukikacha kikosi hicho cha washika bunduki akikataa kuanzia benchi.
Kuondoka kwa Cech kwenye kikosi cha Chelsea, hiyo inamaanisha pia kocha wa magolikipa Christopher Lollichon ataambatana nae kuelekea Arsenal.
Nahodha wa Chelsea John Terry amewaambia mashabiki wa Arsenal kuwa, Cech pekee ataisaidia timu yao kuvuna pointi 12 hadi 15 ndani ya msimu mmoja.
Cech amekipiga Stamford Bridge kwa muda wa miaka 11, Terry ameuambia mtandao mmoja wa michezo (Talk SPORT) kuwa, sasa Arsenal wanaweza wakawania ubingwa na siyo nafasi ya pili kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa muda mrefu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox