MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana, Asamoah Gyan amejitolea kulipa gharama za matibabu kwa wagonjwa moyo katika kituo kikubwa cha maradhi hayo nchini humo.
Ikiwa imepita wiki moja toka Gyan ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo kuwaongoza wachezaji wenzake kutoa msaada wa dola 11,000 kwa wahanga wa mlipuko wa moto na mafuriko yaliyotokea jijini Accra.
Baada ya timu ya taifa kuididimiza Mauritius kea mabao 7-1 katika mchezo wao wa kwanza wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2017, Gyan alitoa msaada wake huo katika hospitali ya Cardio kikiwa ndio kituo kikubwa nchini humo.
Kabla ya kutoa msaada huo ambao unakadiriwa kufikia dola 10,000, Gyan alikwenda kwanza kumtembelea kocha wake wa zamani Nii Noi Thompson ambaye amefanyiwa upasuaji kurekebisha pingili za mgongo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni