TIMU ya taifa ya Serbia wametawadhwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya Kombe la Dunia kea vijana chini ya umri wa miaka 20 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 waliopata katika mchezo fainali dhidi ya Brazil uliofanyika jana.
Bao la ushindi la Serbia liliwekwa kimiani na Nemanja Maksimovic katika dakika ya 118 baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa North Harbour uliopo huko Auckland, New Zealand.
Nchi ambayo ilijitenga kutoka kwa Yugoslavia mara ya mwisho kushinda taji hilo ilikuwa nchini Chile mwaka 1987.
Katika mchezo mwingine wa kutafuta mshindi wa tatu Mali walifanikiwa kuwanyuka Waafrika wenzao Senegal waliocheza pungufu kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kunyakuwa nafasi hiyo.
Mchezaji bora wa mashindano ni kijana kutoka Mali ambaye pia anakipiga kunako timu ya Lille ya Ufaransa Adama Traore mwenye umri wa miaka 19
Na kwa upande wa ufungaji bora tuzo hiyo imekwenda kwa kijana kutoka Ukraine Viktor Kovalenko mwenye miaka 19 aliyefunga mabao - 5 goals, na amesaidia mabao mengine 2. Lakin alikumbana na upinzani mkali kutoka kutoka kwa mchezaji wa Bence Mervo kutoka Hungary ambaye naye alifunga mabao – 5 goals, lakini hakutoa assists hata moja hali iliyopelekea kijana huyo kutoka Ukraine kuchukua kiatu cha dhahabu
Golikipa kutoka Serbia Predrag Rajkovic, ndiye aliyechukua tuzo ya mlinda mlango bora wa mashindano baada ya kufungwa magoli manne kwenye michezo saba aliyokaa golini
Timu ya Ukraine imekuwa timu yenye nidhamu katika mashindano hayo (FIFA Fair Play Award)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni