JUVENTUS YASAJILI MKALI WA MABAO MUARGENTINA
KLABU ya Juventus imekamilisha usajili wa mshambuliaji Murgentina, Paulo Dybala kutoka Palermo kwa dau la Pauni Milioni 24.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa anahusishwa na kuhamia Chelsea,
Manchester United na Arsenal baada ya kuwa msimu mzuri Italia, ambako
amefunga mabao 13 katika mechi 35 za Ligi.
Lakini
amechagua kubaki Italia na amesaini Mkataba wa miaka mitano na 'KIbibi
Kizee' cha Turin, kwa sababu walionyesha dhamira haswa ya kumsajili na
kuamua kuipotezea Ligi Kuu ya England.
tovuti ya klabu hiyo imesema:
"Juventus Football Club inaweza kutangaza kufikia makubaliano na
Palermo juu ya huduma za Paulo Dybala, ambaye amesaini Mkataba wa miaka
mitano.
Akizungumza baada ya uhamisho huo, Dybala alisema kwamba: "Juventus ni klabu ambayo ilikuwa inanihitaji mimi zaidi. "Walifanya jitihada za dhati kunisajili na ndiyo maana nimefanya uamuzi,".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni