MAKOMBE 24 MPAKA SASA KWA XAVI JE KUONGEZA LA 25?
Wakati Xavi Harnandez ,35, anajiandaa na kustaafu rasmi
baada ya kuitumikia Barcelona kwa miaka 17 ya maisha yake, swali je,
atafanikiwa kuongeza kombe jingine hapo keshokutwa.
Barcelona inashuka dimbani mjini Berlin, Ujerumani
kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus ya Italia.
Utaona katika picha hiyo hapo juu, Xavi akiwa
amezungukwa na makongwe 24 aliyowahi kubeba akiwa na Barcelona kwa miaka 17.
Hapo kuna makombe manane ya La Liga, matatu ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya, mawili ya UEFA Super Cups, matatu ya Copa del Reys, sita ya
Spanish Supercups na mawili ya Kombe la Dunia kwa klabu.
JE! ATAWEZA KUBEBA UBINGWA WA 25 NDANI YA BARCA KABLA AJASEPA?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni