KOCHA wa timu ya taifa ya Uruguay, Oscar Tabarez amekiri mipango yake ya kuizuia Argentina jana katika mchezo wao wa Copa America ilivurugwa kea uwezo mkubwa wa Lionel Messi.
Tabarez amemuelezea nyota huyo wa Argentina kama bingwa wa kucheza na mpira kutokana na uwezo mkubwa alioonyesha katika mchezo huo.
Mchezo huo wa kundi B uliamuliwa na bao pekee lililofungwa na Sergio Aguero katika dakika ya 56 ya mchezo lakini Uruguay ambao ndio mabingwa watetezi wangeweza kupata walau sare kutokana na kosakosa walizopata dakika za mwishoni kupitia kea Diego Rolan na Abel Hernandez.
Hata hivyo, Tabarez anadhani Messi alionyesha tofauti kati ya pande hizo mbili na kuongeza kuwa kikosi chake kilikosa mbinu mbadala ya kukabiliana na ubora wa mchezaji huyo.
Akihojiwa Tabarez amesema walijiandaa vyema kea ajili ya mchezo huo lakini Messi siku zote huwa hatabiriki kwasababu huwezi kujua atakifanya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni