STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 17 Juni 2015

TAIFA STARS YAZOMEWA KARUME, KUONDOKA KESHO KWENDA ZANZIBAR KUCHEZA NA UGANDA



TIMU ya Taifa ‘Taifa Stars’ leo  asubuhi ilionja adha ya kuzomewa na mashabiki kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ilipokwenda kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa ma mchezo wa kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.

Taifa stars iliwasili uwanjani hapo saa 3:30 asubuhi  na kukuta mashabiki wakiangalia mazoezi ya Yanga ambayo inajiandaa na mashindano ya Kagame yanayotarajia kuanza Julai, 9.

Baada ya kuwasili  meneja wa timu hiyo Boniface Clemence alianza kushusha vifaa vya mazoezi na wachezaji kuanza kushuka, mashabiki walipowaona ndipo wakaanza kupiga kelele za kuzomea huku wengine wakiwaita watalii hali iliyofanya kocha kuamuru vifaa virudishwe ndani ya gari.
“Buuuh watalii hao, buuu watalii hao,” walizomea mashabiki hao.

Kelele hizo ziliongezeka kwani mashabiki waliokuwa kwenye jengo la Machinga nao walipowaona walizomea zaidi.
Baadae zomeazomea hiyo ilikuja kutulizwa na meneja Clemence pamoja msaidizi wa rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi Juma Matandika waliowataka mashabiki kuwa wazalendo kwani hiyo ni timu yao ya taifa hakuna haja kuizomea.

“Jamani mnapozomea haisadii kwani hii ni timu yetu sote watanzania ni kweli tumefungwa lakini angalia rekodi ya Misri, hakuna timu ambayo imekwenda kucheza pale ikatoka bila kufungwa tena kwa idadi kubwa ya mabao,”, alisikika akisema Clemence.

Baada ya hali kuwa shwari wachezaji na benchi la ufundi walitoka wakaingia Uwanjani kuanza mazoezi huku wakipishana na Yanga ambao nao walikuwepo kwenye Uwanja wa Karume wakifanya mazoezi.

Taifa stars inatarajiwa kuondoka leo kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda utakaochezwa keshokutwa.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Taifa Stars Mart Nooij alisema anaamini watashinda kwani wachezaji wake wapo vizuri kuanzia mbinu, akili na morali ipo juu kwani wanajua wana deni kwa watanzania.
“Naamini tutashinda kwani tumejiandaa kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji wameshasahau yaliyopita tunachoomba ni ushirikiano kwa watanzania wote”, alisema Nooij.

Aidha, rais Malinzi amemwambia kocha huyo kuwa akishindwa kuivusha timu  katika michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani  (CHAN) kibarua chake kitaota mbawa.
Baada ya mchezo huo wa Jumamosi, mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda utachezwa Julai 4, mwaka huu nchini Uganda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox