Yamesemwa mengi sana ila mwisho
wa siku leo ndo leo asemae kesho ni muongo kila pande imejigamba wana wa
Blaugrana vilevile Vecchia Signora wa
Turin mimi yangu macho si hitaji kujiita mkwezi mbele ya kambi ya wakwezi
ukweli wa mambo ni Olympiastadion kwenye msimu wa 60 wa mashindano ya vilabu
barani Ulaya na msimu wa 23 tangu muangazo mpya wa mashindano haya.
Mwamuzi wa mchezo huo ni CUNETY
CAKIR atakaesimama katika dimba la
Olympia stadion ndani ya Jiji Berlin ana umri wa miaka 38 akiwa amezaliwa
huko Instabul,Uturuki 23/11/1976 , amechezesha zaidi ya michezo 170 huku mchezo
wake wa kwanza wa uefa champions
league ulikuwa kati ya Skonto fc vs
Sliema wanderers julai 2003 kama kamisaa
Aidha sept 29 2010 alichezasha mcheza wa
Cl hatua ya makundi kati ya Rubin Kazan na FC
Barcelona mchezo huo uliisha kwa timu zote kutokufungana , pia
alichezesha mchezo kati ya Chelesea na Spartak Moscow.
Raia huyu wa Uturuki pia
atakumbukwa kwa kumpiga kadi nyekundu John Terry katika kipindi cha kwanza kwenye nusu fainal ya uefa kati ya
Chelsea na Barcelona mchezo
ulioisha kwa sare ya 2-2 na kushuhudia
Chelsea akitinga fainal na kubeba kombe hilo chini ya Roberto Di Mateo, bila
kusahau mchezo wa Manchester utd dhidi ya Real madrid ambapo atakumbukwa na
mashabiki wa United kwa kitendo cha kumpa Luis Nani kadi nyekundu kumbuka game
hiyo ndo ilikuwa ya mwisho kwa Mzee Ferguson kwenye Uefa.
kwa maana hiyo michezo yote ya
fc barcelona aliyo chezesha timu hiyo ilitoka sare ingawa leo haito lala kitanukishwa
mpaka kieleweke
MALDIN
FC BARCELONA;
Walikuwa vinara katika group F'
kwa jumla ya pointi 15 ,kwenye hatua ya 16 bora walikipiga dhidi ya Manchester
City na waliibuka na ushindi wa jumla goli 3-1, robo fainal wakacheza
dhidi Paris Saint-Germain napo
hawakufanya makosa kwa kuwachambanga mabingwa hao wa Ufaransa kwa jumla ya goli 5-1, upande wa nusu fainal
walipambana na 'The Bavarian' chini ya
kocha wao wa zamani Pep Guardiola mwisho wa siku walifanikiwa kuwachapa goli
5-3 ushindi wa jumla na baada ya hapo wakafudhu hatua ya fainal .
Mpaka sasa Blaugrana wamefunga
jumla ya magoli 28 kinara wa magoli ni Lionel Messi mwenye magoli 10 ndani ya
dakika 1057 alizocheza, Neymar anamagoli 9 kwenye dakika 936 alizo kipiga, Luis
Suarez kapachika magoli 6 katika dakika 737 alizo cheza kwa maana hiyo safu ya
ushambuliaji ya Barcelona MSN-KOMBINENGA,KOMBINESHENI DE AMERICA ina jumla ya magoli 25.
JUVENTUS;
Kibibi kizee walikuwa group A'
kama washindi wa pili kwa pointi 10 ,hatua ya 16 bora walikwaana na Borussia
Dortmund na kuibuka na ushindi wa jumla 5-1 ,kisha waka kwea hadi robo fainal
wakakipiga dhidi ya Monaco ya kule nchini Ufaransa na mwisho wa siku wakaibuka
na ushindi wa jumla goli 1-0 walilo lifunga pale Turin, baada ya hapo wakajivinjari mpaka hatua ya nusu fainal
wakakumbana na mabingwa watetezi Real Madrid mechi ambayo asilimia kubwa ya
wapenda soka waka anza vuta taswira ya Real kupata mteremko kuelekea fainal na
huenda wangetetea ubingwa wao ila mwisho wa siku umzaniae kumbe ndie sie
mbwembwe za soka huwa dimbani kibibi kizee kikaibuka na ushindi wa jumla magoli
3-2 baada ya hapo tunawashuhudia kwenye fainal ya msimu huu.
Vecchia Signora wao upande
wao wana jumla ya magoli 16 kinara wao wa magoli ni Carlos Tevez mwenye magoli
7 ndani ya dakika 1066 alizo cheza
anaemfuata ni Alvaro Morata anmagoli 4 kwenye dakika 659 alizo kipiga na Artulo Vidal mwenye goli 1 katika dakika
966 kwa mantiki hiyo MTV UTATU WA TURINI unajumla ya magoli 12 pekee.
KUMBUKA
* Vilabu vya Uhispania na Italia vimekutana
mara 44 tumeshuhudia sare 11, Hispania wakishinda mara 18 , Italia waki ibuka
na ushindi marav 15.
* Barcelona wamekutana mara 8 na Juventus
kwenye michuano ya barani ulaya , Juventus wameshinda mmichezo 4, Barcelona
wakaibuka na ushindi katika michezo 2 na kushuhudia sare 2 mara zote walizo
kutana Juventus walifunga jumla ya magoli 10 kati ya 9 ya Barcelona.
* Juventus wamepoteza
fainali 3 zilizo pita mara ya mwisho kushinda ni fainali ya msimu wa 1995/96
mbele ya Ajax wakati wapinzani wao Barcelona wameshinda fainal zao 3 zilizo
pita mara ya mwisho kupoteza ni fainali ya msimu wa 1993/94 dhidi ya Ac Milan.
* Ni fainali ya 7 kwa timu
za Hispania na Italia kukumbana na
fainali zilizo pita timu za Italia zimeshinda mara mbili dhidi ya timu za
Uhispania .
*Endapo Barcelona watwaa ubingwa
huu utakuwa wa 5 na hivyo kuwa timu pekee iliyo twaa ubingwa huu mara nyingi
zaidi tangu msimu mpya wa uefa uanze 1992.
*Patrice Evra atakuwa
mchezaji wa pili kucheza fainali tatu za mashindano haya kwenye timu 3
tofauti (Monaco, Manchester United na
Juventus), atakuwa sawa na injini ya kiholanzi
Clarence Seedorf aliecheza fainali akiwa na ( Milan, Ajax na Real
Madrid).
* Timu zote zimetwaa vikombe viwili kwenye ligi
zao za ndani Juventus wakichukua ubingwa wa ligi kuu nchini Italia Seria A
pamoja na Coppa Italia wapinzani wao Barcelona wamechukua ubingwa wa kombe la
mfalme na ligi kuu almarufu kama La-liga. hivyo kila upande unatafuta trebo kwa
udi na uvumba .
MR'CHOI -KONA KALI- Kwa kuangazia pande zote kila timu ina ubora wake tuna
wazungumzia Juventus ikiwa timu yenye viungo bora kabisa ambao wanasaidiana
vyema na safu ya ulinzi katika upande wa kujihami bila kusahau mashambulizi yao
ya kustukiza kwa kutumia vyema kasi ya Tevez kwa kumpitishia mipira hatarishi ,
Allegri kaunda kikosi kinacho jua kupambana katika engo zote hawa ndo roho yake Claudio Marchisio ,Paul
Pogba,Andrea Pirlo na Arturo Vidal sasa
ukijaribu kuangaza ni viungo bora mbele ya viungo wa Barca wabishi kwenye kila
kona ama unaweza sema hawarembi.
Kuelekea kwenye mchezo wa leo
shughuli pevu itakuwa kwa Claudio
Marchisio na Paul Pogba kudili na Jordi Alba pamoja na Daniel Alves
watu ambao pande zao ndo huwa kuna madhara kwa mantiki ya mipira mingi
ya Barcelona pasi huchezwa pembeni
asilimia 27.6 upande wa kulia na upande wa kushoto
asilimia ni 26.8.
Iko wazi hawataweza shindana
kumiliki mpira na Barca kwa maana hiyo uwepesi wa mashambulizi ya kustukiza,
mpira wa kasi ndo silaha kubwa moja ya madhaifu ya Barcelona ni mipira ya juu
kitu ambacho kinaweza wapa faida pindi wakipa kona na kutupia krosi .
Uwepo wa Andrea Barzagli kwa maana
ya kutokuwepo kwa Giorgio Chiellini
haina maana safu ya ulinzi ya Juventus na cha kufanya ni kuziba njia kwenye
zone yao pindi wakishambulia kwa maana Barcelona ni hatari sana kutokana na
mpaka sasa magoli yao 28 takribani magoli 25 wamefunga ndani ya box bila
kusahau faulo zisizo na mantiki.
Barcelona wao liko wazi
Neymar amekuwa akipoteza nafasi nyingi sana kwa uzembe amekuwa na utoto mwingi
kitu ambacho anatakiwa akiepuke siku ya leo zaidi ya hapo kwa pale mbele wako
vyema tatizo kubwa licha ya msimu huu kuimalika kwenye safu ya ulinzi ila bado
wamekuwa si wazuri katika mipira ya juu hasa upande wa kumaki watu zaidi ya
hapo ni kwa wao kuto lememaa sana pindi wakiwa na umiliki wa mpira kwa mantiki
ya kutokuweka nafasi ya kushambuliwa kwa kustukizwa pindi wakipoteza mpira.
UBASHIRI-Kwa kuangazia pande
zote na dizaini ya mchezo utakavyo kuwa kwa maana ya upande mmoja kumiliki
zaidi na mwingine kumiliki kwa maana ya mashambulizi ya kustukiza nawapa nafasi
Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 2-1 magoli ya pande zote yatafungwa na
wachezaji wa bara la Amerika.

MALDIN
JE NI MESSI,SUAREZ,NEYMAR
NIKIMAANISHA MSN KOMBINENGA DE AMERICA AU NI MTV YAANI MORATA,TEVEZ,VIDAL tuta waaga kesho maana bado kuna jambo
KWA MAONI;
choikangta.ckt@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni