MIAMBA
ya kandanda ya Hispania, FC Barcelona imefanikiwa kutwaa kombe la tano
la Uefa Champions League baada ya kushinda 3-1 dhidi ya mabingwa wa
Italia, Juventus katika mechi ya fainali iliyopigwa jana usiku uwanja wa Olympic, mjini Berlin, Ujerumani.
Barcelona
walianza mchezo kwa kasi huku wakigongeana pasi za uhakika na katika
dakika ya tatu, Ivan Rakitic aliandika bao la kwanza akimalizia pasi
murua ya Andres Iniesta.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi
cha pili Juventus walijipanga na kusawazisha goli hilo kupitia kwa
Alvaro Morata aliyemalizia mpira uliotemwa na golikipa kutokana na shuti
kali la Carlos Tevez.
Dakika
ya 68' Lionel Messi alipiga shuti kali lililotemwa na kipa wa Juve,
Buffon na mpira kumkuta Luis Suarez aliyefunga goli ta pili na la
ushindi.
Suarez
alimalizia kwa haraka mpira uliotemwa na Golikipa Gianluigi Buffon
kutokana na shuti kali la Lionel Messi na kuandika goli la pili kwa
Barcelona.
Suarez akishangilia goli lake
Wachezaji wa Barcelona wakijiandaa kwenda kushangilia goli la kwanza la Ivan Rakitic
Andrea Pirlo na Paul Pogba waliishia kumtazama kwa macho Rakitic' akimuadhibu Gianluigi Buffon
Rakitic ni moja ya mashujaa leo
Neymar
alifunga goli la tatu na kuipa Barcelona taji la nne la Uefa ndani ya
muongo mmoja, lakini huku nyuma waliwahi kubeba mara moja.
Neymar akishangilia baada ya kipyenga cha mwisho
Goli
kipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen akilala bila mafanikio baada
ya kufungwa goli na Morata, kufuatia kuutema mpira uliotokana na shuti
kali la Carlos Tevez.
Gerard
Pique, Carlos Tevez, Dani Alves, Jordi Alba , Pirlo na Rakitic
walibaki midomo wazi wakati, Mhispania huyo akiandika goli la
kusawazisha
Morata, ambaye alifunga pia dhidi ya Real Madrid katika mechi zote mbili za nusu fainali aliendelea kuwa moto wa kuotea mbali
Rakitic na Neymar wakishangilia goli la kwanza
Rakitic, Neymar, Andres Iniesta na Lionel Messi wakishangilia goli la kwanza
Rakitic akizingirwa na wenzake baada ya kufunga goli
Dakika za nyongeza, Neymar akaifungia Barcelona goli la tatu kutokana na shambulizi la kushitukiza.
Barcelona chini ya Luis Enrique wamefanikiwa kutwaa makombe matatu msimu huu kwani awali walitwaa La Liga na kombe la Mfalme 'Copa del Rey'.
Hakika msimu wa 2014/2015 ulikuwa mgumu kwa walinzi wa timu za La Liga na Uefa Champions League kwasababu moto wa Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar Jr ni sawa na wa Petroli usiozimwa kwa maji.
TAKWIMU ZA MECHI YA LEO, BARCA KULIA, JUVENTUS KUSHOTO
statistics :
7
Barcelona chini ya Luis Enrique wamefanikiwa kutwaa makombe matatu msimu huu kwani awali walitwaa La Liga na kombe la Mfalme 'Copa del Rey'.
Hakika msimu wa 2014/2015 ulikuwa mgumu kwa walinzi wa timu za La Liga na Uefa Champions League kwasababu moto wa Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar Jr ni sawa na wa Petroli usiozimwa kwa maji.
TAKWIMU ZA MECHI YA LEO, BARCA KULIA, JUVENTUS KUSHOTO
statistics :
7
shots on target
8
8
shots off target
10
38
possession (%)
62
8
corners
6
1
offsides
0
24
fouls
12
2
yellow cards
1
14
goal kicks
9
1
treatments
1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni