KIUNGO wa Arsenal, Tomas Rosicky amekiri kuzungumza na Petr Cech kuhusu mustakabali wake na kudai kuwa sio siri kuwa golikipa huyo wa Chelsea anataka kuondoka kipindi hiki cha kiangazi.
Cech mwenye umri wa miaka 33 anataka kuondoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu baada ya kuitumikia kea miaka 11 huku Arsenal ikiwa ndio klabu inayotajwa kea nyota huyo kutaka kwenda.
Manchester United na Paris Saint-Germain pia zimekuwa zikihusishwa na tetesi za kumtaka Cech ambaye anataka familia yake iendelee kubakia jijini London.
Akihojiwa katika uzinduzi wa jezi mpya za Arsenal kwa ajili ya msimu ujao Rosicky amesema hataki kudanganya kwakuwa in kweli amezungumza na Cech kuhusu mustakabali wake kwasababu sio siri kuwa anataka kuondoka.
Hata hivyo Rosicky hakuweka wazi mahali gani haswa Cech atakwenda akidai kuwa amepewa ofa na timu nyingi lakini mwenyewe angependelea zaidi kubakia jijini London kea ajili ya familia yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni