STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 2 Julai 2015

CHICHARITO AVUNJIKA BEGA.

MSHAMBULIAJI nyota w Manchester United, Javier Hernandez anatarajiwa kuikosa michuano ya Gold Cup kufuatia kuvunjika kwa mfupa wa bega. 

Hernandez alipata majeraha hayo wakati alipogongana na Brayan Beckeles katika mchezo wa kujipima nguvu wa Mexico waliokuwa wakicheza dhidi ya Honduras katika dakika ya 41 na nafasi yake kuchukuliwa na Oribe Peralta. 

Daktari wa timu Gerardo Aguilar alithibitisha majeruhi hayo ya Hernandez na kuongeza kuwa anatarajiwa kukaa nje kwa kipindi cha wiki tatu mpaka nne. Kocha wa Mexico Miguel Herrera amesema kuumia kwa mshambuliaji huyo ni pigo kubwa kwa kikosi chake kuelekea katika michuano hiyo. 

Hernandez amefunga mabao 40 katika mechi 74 alizoichezea Mexico akiwa anashika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora katika historia ya nchi hiyo akitanguliwa na jared Borgetti mwenye mabao 46.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox