STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 2 Julai 2015

MOURINHO AUNGA MKONO CECH KWENDA ARSENAL.

UHAMISHO wa golikipa wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, Petr Cech kutoka kwa mabingwa wa Ligi Kuu Chelsea kwenda kwa mahasimu wao wa jiji Arsenal umeungwa mkono na meneja wake Jose Mourinho. 

Cech aliyekuwa golikipa wa Chelsea kwa kipindi cha miaka 10 lakini akapoteza nafasi hiyo mbele ya golikipa wa kimataifa wa Ubelgiji Thibaut Courtois msimu uliopita alijiunga na mapema Jumatatu. 

Mourinho amesema alikuwa anataka Cech mwenye umri wa miaka 33 abakie Chelsea msimu ujao lakini kutokana na kupiteza nafasi yake na mwenyewe kutaka kuondoka alikuwa hana jinsi zaidi ya kumuunga mkono. 

Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Cech amekuwa mtumishi mzuri wa Chelsea kwa kipindi cha miaka 11 ambapo ameisaidia klabu hiyo kushinda kila kitu hivyo anamshukuru kwa kuwa sehemu ya mafanikio hayo. 

Cech ambaye aliibuka Chelsea kwa mara ya kwanza chini Mourinho Agosti mwaka 2004, amefanikiwa kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu, moja FA na lingine la Kombe la Ligi chini ya Mreno huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox