STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 20 Julai 2015

FIFA YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI













Shirikisho la soka Duniani, FIFA limetangaza kwamba uchaguzi mkuu wa Rais utafanyika Februari 26 mwakani.

Maamuzi haya yamefanyika leo katika kikao cha kamati ya utendaji ya Shirikisho hilo kilichofanyika mjini Zurich, Uswisi.

Sepp Blatter aliyejiuzulu siku nne baada ya kuchaguliwa amethibitisha kuwa ataendelea kukaa madarakani mpaka uchaguzi mkuu utapofanyika kupata mrithi wake.


Wakati huo, kundi la watu wanaoshinikiza  kufanyika kwa mageuzi wamekutana leo mjini humo wakimuomba katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan kuongoza mapinduzi hayo.

Kundi hilo limesema Annan ni mtu makini ambaye anapaswa kuongoza tume ya mageuzi wakati  huu Dunia ikielekea kupata mrithi wa Sepp Blatter aliyejiuzulu Urais kutokana na kashfa nzito ya rushwa iliyokumba FIFA.

Shirika la Ujasusi la Marekani, FBI liliwatia mbaroni Maafisa saba wa ngazi za juu wa FIFA kwa tuhuma za rushwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox