STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 20 Julai 2015

MANCHESTER UNITED KUTENGA €100M KUMTWAA MSHAMBULIAJI HUYU



Kwa muiibu wa chombo cha habari cha Ujerumani cha Sport1, Manchester United wanajiandaa kutuma ofa mpya kumsajili nyota wa Bayern, Thomas Muller.

Awali Man United waliweka mezani ofa ya Euro milioni 82 kuinasa saini ya mshindi huyo wa kombe la Dunia 2014, lakini Miamba ya Bavarian ilikataa.

Wakiwa tayari wamemsajili Gwiji wa Bayern, 
Bastian Schweinsteiger,  Louis van Gaal anajiamini kwamba anaweza kumsajili Muller.

Sport1 wanadai kwamba United wapo tayari kulipa Euro milioni 100 sawa na paundi milioni 69 kumsajili Muller.

Dau hilo limeandaliwa na bosi mwenyewe Ed Woodward.

Kama United watamsajili kwa dau hilo, utakuwa usajili ghali zaidi kuwahi kufanyika na klabu hiyo wakivunja rekodi ya kumnasa Angel Di Maria kwa paundi milioni 59.7 majira ya kiangazi mwaka jana.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge 
amewaondoa hofu mashabiki kwamba hakuna mchezaji atakayeuzwa kwa sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox