STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 18 Julai 2015

REAL MADRID NA MANCHESTER UNITED VUTA NIKUVUTE


Manchester United  wanajiandaa kumuachia David De Gea kama mchezaji huru msimu ujao kuliko kumuuza kwa sasa kwenda Real Madrid.

Man United wameweka masharti kwamba De Gea atauzwa Real Madrid majira haya ya kiangazi endapo miamba hiyo ya Bernabeu itakubali kuwauzia mlinzi wa kati, Sergio Ramos.

Kumbuka De Gea na Ramos wote wapo katika timu zao kujiandaa na msimu mpya.

Kocha mpya wa Real Madrid, Rafa Benitez amesema hataki tu Ramos abakie Bernabeu bali anataka kumpa kitambaa cha unahodha kufuatia Iker Casillas kuondoka.

Kwa mujibu wa The Guardian, inasemekana dili la Ramos kutua Old Trafford linaweza kukamilika kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Majira ya kiangazi.

United hawana presha ya kuuza wachezaji kwenda klabu kama Real Madrid kwasababu wana mkwanja wa kutosha kuweza kuwazuia wanasoka wake.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox