STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 18 Julai 2015

YANGA YAPOKEA KICHAPO,APR YAFANYA KWELI

WENYEJI Yanga SC, leo wameanza vibaya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kufungwa mabao 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kipigo cha Yanga SC leo kwa kiasi kikubwa kilichangiwa na kucheza pungufu kwa zaidi ya dakika 65, kufuatia mshambuliaji wake, Mzimbabwe Donald Ngoma  kutolewa kwa kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza.



















Yanga waliuanza vizuri mchezo huo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya tano tu kupitia kwa Ngoma aliyepiga mpira mrefu kama krosi kutoka upande wa kushoto na kutinga nyavuni, huku beki Harun Shakava akiusindikiza kwa macho.

Winga Simon Msuva alichangia kuwatibulia hesabu za kuokoa Shakava na kipa wake, Boniface Olouch kutokana na kuifuatilia vizuri krosi ya Ngoma hadi inatinga nyavuni. 

Bao hilo halikudumu sana, kwani Gor Mahia walifanikiwa kusawazisha dakika ya 18 kupitia kwa na Dirkir Glay aliyepiga shuti kali la mpira wa adhabu lililomshinda kipa Ally Mustafa ‘Barthez’.

Faulo hiyo ilitolewa baada ya beki wa kulia, Juma Abdul kumuangusha Godfrey Walusimbi nje ya boksi.

Refa Ssali Mashood alimtoa nje kwa kadi nyekundu Mzimbabwe, Ngoma baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumsukuma Shakava wa Gor baada ya kumpamia na mpira hadi nje ya Uwanja dakika ya 25.

Yanga SC walitulia baada ya kumpoteza Ngoma aliyeondoka uwanjani analia na kuanza kucheza kwa tahadhari kuwanyima nafasi Gor, hali ambayo ilisaidia dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizike timu hizo zikiwa zimefungana 1-1.  












Kipindi cha pili, Gor Mahia waliingia na mashambulizi ya kulazimisha na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya kwanza tu kupitia kwa mshambuliaji wake, Michael Olunga, aliyewapiga chenga mabeki wa Yanga kabla ya ‘kufyatua’ shuti lililompita Barthez.

Yanga SC walipoteza nafasi nzuri ya kupata sare dakika ya 73, baada ya Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumdakisha mkwaju wa penalti kipa Oluoch, kufuatia Shakava kuunawa mpira kwenye boksi.


















Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga, kwa ujumla, Yanga SC iliathiriwa na kucheza pungufu.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Joseph Zuttah dk75, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Simon Msuva/Kpah Sherman dk69, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Salum Telela dk84. 

Gor Mahia; Boniface Olouch, Mussa Mohammed, Sibomana Abouba, Harun Shakava, Kari Nzigiyimana, Dirkir Glay, Khalid Aucho/Erick Ochieng dk89, Godfrey Walusimbi/Ronald Omino dk86, Innocent Wafula/Enock Agwanda dk86, Medie Kagere na Michael Olunga.




















Wakati  huohuo 
APR ya Rwanda imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Shandy ya Sudan Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa Kundi C, bao pekee la APR lilifungwa na kiungo Bizimana Djihad, dakika ya 64 kwa shuti kali baada ya kupasua katikati ya Uwanja na baada ya kupata upenyo.

Kiungo huyo aliyesajiliwa mapema mwezi huu kutoka kwa mahasimu, Rayon Sport ili kuziba pengo la Jean Baptiste Mugiraneza aliyehamia Azam FC, ni mtoto wa dada wa kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima, ambaye pia aliwika Rayon na APR kabla ya kuja Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox