SIMBA imeamua kukata mzizi wa fitna sasa, imeamua kusajili mshambuliaji wa ‘mauaji’ kutoka nchini Senegal.
Huyo
ni Papa Amadou Niang ambaye anatarajia kutua nchini leo Ijumaa akitokea
Dakar, Senegal kwa Shirika la Ndege la Kenya kwa ajili ya kumalizana na
Msimbazi.
Wakala
wa mchezaji huyo kutoka nchini Cameroon, alitarajia kutua nchini jana
ili kumalizana na uongozi wa Simba mara mchezaji huyo atakapotua.
Taarifa
za uhakika kutoka Dakar zinaeleza Simba imeomba ruhusa ya mchezaji huyo
afanye mazoezi na wenzake kwa siku tatu, pia imepewa nafasi imtumie
katika mechi moja ili kujiridhisha kwa kuwa awali wakala wake huyo
Mcameroon, alikataa asifanye majaribio.
Papa
ambaye imeelezwa ni ndugu wa damu wa mshambuliaji nyota wa zamani na
nahodha wa Senegal, Mamadou Niang ambaye alikuwa akiisumbua Taifa Stars
kila walipokutana nayo, anaelezwa kuwa mmoja wa washambuliaji wenye
kasi.
Taarifa
za uhakika zinaeleza Niang atawasili nchini saa 3:10 asubuhi akitokea
Dakar baada ya kupitia katika miji miwili ya Abidjan, Ivory Coast na
Nairobi, Kenya.
Safari
yake kufika Nairobi kutoka Dakar itakuwa ya saa 10 na dakika 40 na saa 1
na dakika 25 kutoka Nairobi hadi Dar es Salaam. Maana yake atatumia saa
12 na dakika 5, kuifuata Simba ya Dar es Salaam ambayo imemwambia ‘njoo
tuone’.
Moja ya sifa zake kubwa ni kuwatoka mabeki, lakini ana uwezo wa kupiga mashuti makali kwa miguu yote.
Simba
imeamua kujiridhisha na sifa hizo kwa siku ilizopewa ikiwa ni pamoja na
kumtumia katika mechi moja ya kirafiki halafu itachukua uamuzi kama
inambakiza Dar es Salaam au arejee kwao Dakar.
Niang amecheza soka katika nchi za Ulaya kama Kazakhstan ambako aliichezea FC Vistok na kuwa mfungaji bora.
Kabla
ya hapo alikuwa mshambuliaji tegemeo wa kikosi cha FF Jaro cha Finland
ambako alicheza na Mkenya, Peter Opiyo, akafanikiwa kufunga mabao saba
katika mechi nne.
Alijiunga
na Jaro akitokea AC Oulu ya Finland pia, baadaye alikwenda kucheza
Kuwait katika Klabu ya Al Shabab ambayo baadaye ilimuuza CF Mounana ya
Gabon ambayo taarifa zinaeleza mwishoni mwa msimu uliopita, alisusa
kuichezea baada ya ‘kukamatwa’ na ukata na kushindwa kumlipa.
Kocha
Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amekuwa akisisitiza anahitaji straika wa
‘kufia’ nyavuni na kama ataridhika na Msenegali huyo, basi atakuwa
ametimiza kiu yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni