Manchester
United walikuwa ni miongoni mwa klabu ambazo zimetumia kiasi kikubwa
cha pesa kwa ajili ya usajili kwenye dirisha la usajili la majira ya
joto msimu huu.
Wamewasajili wachezaji wenye gharama kubwa lakini pia
walishindwa kuwasajili baadhi ya wachezaji ambao walikuwa kwenye orodha
ya wachezaji ambao waliwahitaji kwa ajili ya kuboresha kikosi chao.
Hii ni orodha ya wachezaji 10 ambao Van Gaal alijaribu kuwasajili lakini hakufanikiwa.
10.Hugo Lorris (Tottenham)
Manchester
United ilijaribu kumsajili golikipa wa Tottenham Hugo Lorris kwa ajili
ya kurithi mikoba ya David De Gea aliyekuwa aikiwindwa kwa karibu na
klabu ya Real Madrid.
Lakini bado mambo hayakwenda sawa baada ya Madrid
kushindwa kumnasa golikipa huyo wa Uhispania.
9.Harry Kane (Tottenham)
Louis
van Gaal aliweka kitita cha Euro milioni 45 baada ya striker wa Spurs
kuonesha kiwango cha hali ya juu na uwezo mkubwa wa kufunga kwenye msimu
uliopita lakini bado deal hilo halikufanikiwa.
8.Arda Turan (Barcelona)
Kwa
mujib wa ripoti kadhaa, kiungo wa zamani wa Atletico Madrid alikuwa
kwenye radar za Manchester United kabla ya kusajiliwa na Barcelona.
7.Neymar (Barcelona)
Manchester
United ni miongoni mwa klabu ambazo mara kadhaa zimekuwa zikitaka
kumsajili nyota huyo wa Barcelona.
Van Gaal alitoa dau kubwa kwa ajili
ya mshambuliaji huyo wakati akifahamu haitakuwa kitu rahisi kumnasa
Neymar.
6.Pedro (Barcelona)
Pedro
alikuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na Manchester United na kila kitu
kilikuwa kinakwenda sawa, lakini walishindwa kufanya hivyo na matokeo
yake akanaswa na Chelsea katika dakika za mwisho.
5.Raphael Varane (Real Madrid)
Louis
van Gaal alitaka pia kuinasa saini ya mlinzi huyu wa Real Madrid Madrid
kwa ajili ya kuipa nguvu safu yake ya ulinzi lakini bado jambo hilo
halikufanikiwa.
4.Sergio Ramos (Real Madrid)
Ramos
ni miongoni mwa mabeki bora wa kati ulimwenguni na Manchester United
walitaka kumsajili ili ajiunge na kikosi chao.
Van Gaal alikaribia
kumnasa lakini katika hatua za mwisho kabisa Ramos akakubali kuongeza
mkataba na kusalia Santiago Bernabeu.
3.Karim Benzema (Real Madrid)
Manchester
United pamoja na Arsenal walikuwa na jina la huyu jamaa kwenye orodha
ya wachezaji wanaohitaji kuwasajili, lakini mwisho wa siku Benzema
ameendelea kubakia Real Madrid.
2.Gareth Bale (Real Madrid)
Kulikuwa
na tetesi kwamba Bale ngesajiliwa na Man United Louis van Gaal pia
alitoa dau kubwa la kueleweka ili kumsaini nyota huyo kwenye majira ya
joto.
Lakini nyota huyo ataendelea kusalia Bernabeu baada ya kuongeza
mkataba wake na Los Bloncos.
1.Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Alikuwa mchezaji namba moja kwenye rada za
Manchester United baada ya mkali huyo wa Ureno kuendeleza makali yake ya
kufunga akiwa Santiago Bernabeu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni