Katibu
mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA, Jerome Valcke amesimamishwa
kuendelea na majukumu yake ili kupisha uchunguzi wa kamati ya maadili ya
FIFA kuchunguza kwa uhakika suala linalomkabili.
Jerome Valcke anakabiliwa na
skendo ya uuzaji tiketi za kombe la dunia kwa magendo. Mfaransa huyo
ambaye aliingia madarakani tangu mwaka 2007 hivi sasa atafanyiwa
mahojiano na polisi wa Zurich na kamati ya maadili ya FIFA.
FIFA chini ya rais aliyejiuzulu
Sepp Blatter ipo katika kashifa nzito za rushwa tangu mwezi Mei mwaka
huu, huku maafisa usalama wa Marekani wakiwashikilia maafisa saba wa
shirikisho hilo kwa tuhuma za rushwa.
Jerome Valcke ambaye ni namba 2
wa Sepp Blatter alitarajiwa kusimama kama rais wa shirikisho hilo baada
ya Blatter kuondoka, lakini hivi sasa yuko kikaangoni kwa mahojiano
zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni