STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 5 Septemba 2015

NIGERIA CHUPUCHUPU KWA STARS WAAMBULIA SARE YA BILA KUFUNGANA


Timu ya taifa ya soka Taifa stars imetoka sare ya bila kufungana na Nigeria katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki mataifa ya Afrika mwaka 2017, mchezo ulichezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa leo Stars waliuwanza mchezo taratibu sawa na Nigeria huku kasi ya mchezo ikiongezeka kadri ya muda unavyoenda.

Taifa stars katika kipindi cha kwanza walitengeneza nafasi 3 za kufunga goli kupitia kwa Mrisho Ngassa na Mbwana Samata ambapo mashuti yao uliishia mikononi mwa kipa wa Nigeria.

Taifa stars wakicheza katika soka la uhakika katika kipindi cha pili walitengeneza nafasi ya 4 za kufunga goli kupitia kwa Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngassa na John Bocco ambao walishindwa tena kuzitumia nafasi hizo.

Nigeria na walifanikiwa kutengeneza nafasi mbili kipindi cha pili na 3 katika kipindi cha kwanza lakini uimara wa Ally Mustapha Bathezi ulizizuia hatari hiyo.

Pamoja na kuwa na maumbo madogo kiungo Mudathir Yahya na Himid Mao walicheza vyema na hata alipoingia Said Ndemla kuchukuwa nafasi ya Mudathiri uimara katika safu ya kiungo ulionekana.

Ngassa na Farid Mussa Maliki leo hawakuwa na siku nzuri ya mchezo japo hawakucheza vibaya sana.

Stars leo iliundwa na: Ally Mustapha, Shomari Kapombe, Hajji Mwinyi, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Himid Mao,Thomas Ulimwengu,  Mudathir Yahya/Said Ndemla 62, Mrisho Ngassa/John Bocco 69, Mbwana Samata, Farid Mussa/Saimon Msuva 83

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox