Kikosi cha Nigeria katika moja ya mechi zao |
Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limetangaza rasmi kuwa kikosi cha Super Eagles kwa ajili ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Taifa Stars kitaondoka Abuja kesho saa 9 jioni kwa saa za Nigeria (saa 7 mchana kwa saa za Tanzania).
Taarifa ya NFF iliyowekwa kwenye mtandao rasmi wa shirikisho hilo jana alasiri, ilisema mabingwa hao mara tatu wa Afrika watatua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 4 usiku kwa saa za Tanzania (saa 2 usiku kwa saa za Nigeria).
Msafara wa Super Eagles utakuwa na wachezaji 23, maofisa wa benchi la ufundi, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya NFF na maofisa wa serikali ya Nigeria, maofisa wa NFF, waandishi wa habari, wadau wa soka wa Nigeria na wajumbe wa klabu ya mashabiki wa soka wa Nigeria.
Nchi hizo mbili hazijawahi kukutana katika michuano hiyo mikubwa barani tangu Desemba 1980, lakini zimekuwa zikichuana katika michuano ya vijana na soka la wanawake katika miaka ya karibuni.
Desemba hiyo ya miaka 35 iliyoipita Taifa Stars ina matumaini ya kufanya kweli kutokana na kuwashika Green Eagles (kipindi hicho) kwa sare ya 1-1 jijini Lagos katika mechi yao ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 1982, lakini magoli mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na John Chidozie na Christian Nwokocha jijini Dar es Salaam wiki mbili baadaye yaliisukuma Tanzania nje ya michuano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni