STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 2 Septemba 2015

BAADHI YA WACHEZAJI WALIOKWAMA KATIKA USAJILI WAO KIANGAZI HIKI.

WAKATI dirisha la usajili majira ya kiangazi likiwa limefungwa jana nchini Uingereza, kuna baadhi ya wachezaji walioshindwa kufanikisha usajili wao katika siku hiyo ya mwisho. 

Mojawapo ya wachezaji walioshindwa kufanikisha uhamisho wao ni pamoja na Edinson Cavani ambaye Arsenal waligoma kulipa kitita cha paundi milioni 50 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyp wa Paris Saint-Germain mwenye umri wa miaka 28. 

Wengine ni mshambuliaji wa West Bromwich Albion Saido Berahino ambaye yeye ameanzisha na mgomo baada ya klabu hiyo kukataa ofa kadhaa zilizotolewa na Tottenham Hotspurs kwa ajili ya kumsajili. 

Mshambuliaji wa Spurs Emmanuel Adebayor mwenye umri wa miaka 31 yeye ilibidi aombe ushauri kutoka kwa padri wake kuhusu suala la kuwindwa na Aston Villa kabla ya kuamua kubakia katika klabu hiyo. 

Nyota wa zamani wa Manchester United Dimitar Berbatov mwenye umri wa miaka 34 naye uhamisho wake wa kurejea katika Ligi Kuu ulidunda baada ya muafaka kushindwa kufikiwa na klabu ya Aston Villa. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox