STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 7 Septemba 2015

SABABU YA MEMPHIS KUTOKUTUMIA JINA LA BABA YAKE KWENYE JEZI YAKE...........



Namba saba: Memphis amechukua namba yenye heshima kubwa katika klabu ya Manchester United.

Baba yake Memphis Depay amemuomba mwanaye kumaliza tofauti zao ili kufungua ukurasa mpya wa maisha.

Nyota huyo wa Manchester United amekataa kutumia jina la ubini kwenye jezi yake kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na baba yake.

Memphis (21), mara zote amekuwa akisikika akisema kwamba baba yake alimtelekeza yeye na familia yake wakati akiwa na umri wa miaka minne.
Lakini baba yake, Dennis amekiri kosa hilo na kumuomba kijana wake amsamehe kwa yote yaliyotokea.

"Kusema kwamba sikumuona tena baada ya ile miaka minne ni uongo", aliliambia gazeti la the Sun.

"Ni kitu kisicho cha kawaida, sio vizuri. Yuke ni kijana wangu na nampenda sana. Mimi ndiye mtu wa kwanza kabisa kupatia mpira wake wa kwanza.

“Hakupewa matunzo mabaya na mimi. Hiyo si kweli.

“Nilimuona kupitia You Tube akiongea kuhusu baba yake, akisema kwamba hakutaka kuweka jina langu kwenye jezi yake. Ilinifanya nijisikie vibaya ana kwa kweli.

“Ningependa siku moja tuwe wote pamoja tena na kijana wangu. Namkumbuka sana kwa kweli”
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox