MENEJA wa Chelsea, Jose
Mourinho ameshitakiwa kwa kuvunja sheria na Chama cha Soka cha
Uingereza-FA kwa kauli yake kwa waamuzi kufuatia kipigo cha mabao 3-1
walichopata kutoka kwa Southampton Jumamosi iliyopita.
Mourinho anadhani
mwamuzi Robert Madley alikataa kuipa penati Chelsea katika mchezo huo
kwasababu aliogopa kufanya hivo.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52
amepewa mpaka Octoba 8 mwaka huu kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kipigo
hicho kinakuwa cha nne kwa mabingwa hao watetezi wa ligi katika mechi
nane walizocheza msimu huu na kuwaacha wakiwa nyuma ya vinara Manchester
City kwa alama 10.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni