Tukio la alhamis la nyota wawili wa Chelsea Diego Costa na Oscar Dos Santos kutaka kugombana baada ya kuchezeana rafu mazoezini wakati wa maandalizi ya mchezo wa kombe la FA jumamosi dhidi ya Scunthorpe United utakaopigwa katika dimba la Stamford Bridge.
Inadaiwa Costa alimchezea rafu mbaya Oscar kisha muda mfupi baadae Oscar akajibu kwa kumkanyaga gotini Costa ambaye alikuja juu akamkwida na kutaka kurushia ngumi kabla ya kuamulia na wachezaji wenzao.
Ingawa Oscar alikanusha kwa wale waliokuwa wanasambaza ujumbe kanakwamba hawapatani na Diego Costa.
Tukio hili ni la pili kuikumba Chelsea baada ya mapema mwezi uliopita Charly Musonda na Cesc Fabregas nao kuwa karibu kugombana baada ya Fabregas kukasirika kufuatia kupigwa tobo na Musonda.
TIZAMA HAPA CHINI BAADHI YA MATUKIO YA KUGOMBANA MAZOEZINI:
Miquel Nelom na Tonny Vilhena wachezaji wa Feyenoord's wakigombana mazoezini walipokuwa kambi Ureno.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni