STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 10 Januari 2016

LEO TAREHE 10, SOMA KILICHOANDIKWA NA MAGAZETI ULAYA KUHUSU USAJILI, MAN CITY YAIVURUGIA MAN U KWA HAZARD...

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Gareth Bale anatarajiwa kukataa maombi ya kutoka Manchester United na Chelsea kufuatia nyota huyo wa kimataifa wa Wales kutaka kuendelea kubakia Santiago Bernabeu.
Chanzo: Sunday People

KLABU ya Manchester United inaripotiwa kujipanga kumchukua meneja wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kama mbadala wa Louis van Gaal, huku meneja wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc naye akitajwa kufikiriwa katika nafasi hiyo.
Chanzo:Sunday Mirror.

KLABU ya Tottenham Hotspurs inajipanga kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy kwa mkopo majira haya ya kiangazi.
Chanzo: Daily Mirror.

KLABU ya Manchester United inataka kitita cha paundi milioni 24 kwa ajili ya Marouane Fellaini lakini hawatakubali kiungo huyo kuondoka kwa mkopo.
Chanzo: Sunday People

KLABU ya Manchester United inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Mainz Yoshinori Muto kwa kitita cha paundi milioni 12.
Chanzo: Sunday Mirror

KLABU ya Manchester City imeingia katika kinyang’anyiro cha paundi milioni 80 na Real Madrid na Paris Saint-Germain kama Eden Hazard ataamua kuondoka Chelsea kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
Chanzo: The Sun

KLABU ya Chelsea inaripotiwa kumuwinda meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ili aweze kuwa mbadala wa Guus Hiddink pindi atakapomaliza muda wake mwishoni mwa msimu huu.
Chanzo: OK Diario

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox