STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 5 Januari 2016

MBWANA SAMATA KUELEKEA NIGERIA KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA NDANI YA AFRIKA

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/05/cover2.jpgKatibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine kesho Jumatano anatarajiwa kuongozana na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta kuelekea nchini Nigeria kwenye sherehe za utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora barania Afrika.

Mwesigwa anatarajiwa kuondoka na Samatta kuelekea Nigeria katika mji wa Abuja ambapo sherehe za utoaji tuzo hizo zitafayika  Alhamisi Januari 7, ambapo siku ya sherehe hizo Katibu Mkuu ataambatana na Ofisa ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria
Mbwana Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAF CL) baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao 8 na kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtakia kila la kheri Mbwana Samatta katika kinyanganyiro hicho cha uchezaji bora na kusema kwa niaba ya watanzania wote wanamuombea dua njema aweze kuibuka mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.


Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox