Katika mchezo huu wa leo Azam FC waliuwanza mchezo vyema na katika dakika ya 16 Ramadhhan Singano kuiandika Azam FC goli la kwanza.
Kuingia kwa goli hilo lilipelekea Azam Fc kutawala mchezo kabla ya Dider Kavumbagu kufunga goli la pili katika dakika ya 42 akimalizia kazi nzuri ya Waziri Salum na kupeleka mchezo kwenda mapumziko Azam wakiwa mbele kwa goli 2-0.
Kipindi cha pili, Ndanda walizinduka na kusawazisha mabao yote – akianza Atupele Green kwa penalti dakika ya 51 baada ya kipa Aishi Manula kuchezea rafu Paul Ngalema ndani ya boksi na refa Ahmad Simba wa Kagera kutenga tuta.
Zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika, Ahmed Msumi alyetokea benchi kipindi cha pili aliifungia Ndanda bao la kusawazisha dakika ya 88 baada ya kufumua shuti la mbali kutokea pembeni na kumbabatiza beki wa Azam Agrey Morris na kutinga wavuni.
Kwa matokeo hayo Azam FC wanajiongezea pointi nyingine moja na kufikisha pointi 52 wakiwa nyuma kwa pointi 5 toka kwa vinara Simba SC na pointi 1 toka kwa Yanga SC.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Waziri Salum/David Mwantika dk46, Aggrey Morris, Racine Diouf/Mudathir Yahya dk46, Serge Wawa, KIpre Bolou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Didier Kavumbagu/John Bocco dk70, Kipre Tchetche na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Ndanda FC: Jeremiah Kisubi, Aziz Sibo, Paul Ngalema, Hemed Khoja, Cassian Ponera, William Lucian, Salum Minelly, Masoud Ally/Burhan Rashid dk20, Omary Mponda/Ahmad Msumi dk85, Atupele Green na Kigi Makassy.
Na katika mchezo mwingine
Jahazi la wagosi wa kaya Coastal union limeendelea kuzama hii leo baada ya kupokea kichapo cha goli 2-0 toka kwa Majimaji FC katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa hii leo katika uwanja wa Majimaji mkoani Songea.
Kwa mujibu wa matokeo hayo coastal union iliyobakiwa na michezo mitano, inaitaji ushindi katika michezo yote hiyo, ili ijihakikishie kubaki ligi kuu ya vodacom kwa msimu ujao.
MSIMAMO WA LIGI KUU BAADA YA MCHEZO WA LEO
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | SIMBA SC | 24 | 18 | 3 | 3 | 43 | 13 | 30 | 57 |
2 | YANGA | 22 | 16 | 5 | 1 | 54 | 12 | 42 | 53 |
3 | Azam FC | 23 | 15 | 7 | 1 | 40 | 16 | 24 | 52 |
4 | MTIBWA SUGAR | 23 | 12 | 6 | 5 | 28 | 16 | 12 | 42 |
5 | T. PRISONS | 25 | 10 | 10 | 5 | 22 | 20 | 2 | 40 |
6 | MWADUI FC | 24 | 9 | 7 | 8 | 23 | 21 | 2 | 34 |
7 | STAND UNITED | 25 | 10 | 4 | 11 | 22 | 22 | 0 | 34 |
8 | MAJIMAJI FC | 25 | 8 | 6 | 11 | 18 | 33 | -15 | 30 |
9 | NDANDA FC | 25 | 5 | 12 | 8 | 22 | 26 | -4 | 27 |
10 | MBEYA CITY | 25 | 7 | 6 | 12 | 27 | 33 | -6 | 27 |
11 | TOTO AFRICANS | 25 | 6 | 9 | 10 | 23 | 34 | -11 | 27 |
12 | KAGERA SUGAR | 25 | 6 | 7 | 12 | 19 | 28 | -9 | 25 |
13 | JKT RUVU | 24 | 6 | 6 | 12 | 24 | 33 | -9 | 24 |
14 | MGAMBO SHOOTING | 25 | 5 | 8 | 12 | 20 | 31 | -11 | 23 |
15 | AFRICAN SPORT | 26 | 5 | 5 | 16 | 10 | 30 | -20 | 20 |
16 | Coastal Union | 26 | 4 | 7 | 15 | 15 | 37 | -22 | 19 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni