STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 8 Aprili 2016

TETESI ZA LEO TAREHE 8 KUHUSU USAJILI ULAYA, WACHEZAJI 8 KWENDA MAN CITY

KIUNGO wa zamani wa Tottenham Hotspurs, Paulinho amepewa ofa na AC Milan wakati klabu hiyo ya Serie A ikijipanga kuimarisha safu yake ya kiungo. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil kwasasa anacheza katika klabu ya Guangzhou Evergrande ya China.
Chanzo: Calciomercato

http://talksport.com/sites/default/files/styles/large/public/field/image/201604/paper_review_-_new.png?itok=jrUWCvAm
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic anadaiwa kujipanga kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na Paris Saint-Germain kabla ya hajakubali ofa ya kitita cha euro milioni 50 kutoka klabu ya Qatar, pamoja na kuwaniwa na klabu za Manchester United na Arsenal.
Chanzo: Gazzetta dello Sport

PEP Guardiola anadaiwa kutaka kuanza kibarua chake Manchester City kwa kusajili wachezaji nane ili aweze kukipangua kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku Aymeric Laporte na John Stones wakiwepo katika orodha yake.
Chanzo: ESPN

KLABU ya Fenerbahce inadaiwa kumuwania winga wa Bayern Munich Franck Ribery kufuatia taarifa kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa anajipanga kuondoka Allianz Arena majira ya kiangazi.
Chanzo: Fichajes.net

KLABU ya Chelsea inajipanga kutoa ofa ya euro milioni 40 kwa ajili ya kiungo wa Bayern Munich Arturo Vidal huku meneja mpya Antonio Conte akidaiwa kuwa na hamu kubwa ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile.
Chanzo: Gazzetto dello Sport

MKURUGENZI wa michezo wa Juventus, Fabio Paratici anadaiwa kwenda jijini Paris Jumatano iliyopita kuwatizama nyota wa PSG Edinson Cavani, Andrien Rabiot na Javier Pastore.
Chanzo: Tuttosport

MENEJA ajaye wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti anadaiwa kutaka kumsajili winga wa Celta Vigo Johnny Castro majira ya kiangazi.
Chanzo: Midi Libre

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox