Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi
mkoani Tabora, Suzana Kaganda aliyesema tukio hilo ni la juzi katika
Mtaa wa Muhaya Kijiji cha Igurubi. Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Sudi
Seif (47).
Alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa
kuwatendea unyama watoto hao, kwa kuwalaghai kuwapa ubuyu na pesa,
endapo wangemkubalia kufanya tendo la mapenzi.
Alisema kwa kuwa watoto hao walikuwa
wadogo, alifanikiwa kuwashawishi, na alianza kwa kumchukua mtoto wa
kwanza mwenye umri wa miaka 5 na miezi 4, anayesoma chekechea Shule ya
Msingi Igurubi.
Kamanda huyo aliongeza kuwa, akiwa
chumbani na mtoto huyo alimwingilia kimwili katika sehemu zote za siri
na kumsababishia maumivu makali hadi wazazi wake walipomgundua wakati
aliporudi nyumbani muda wa jioni.
Alidai kuwa baada ya tukio hilo kwa mtoto
wa kwanza, alimchukua mtoto mwingine mwenye umri wa miaka 9 anayesoma
darasa la pili Shule ya Msingi Ikonda Kata ya Igurubi, aliyemfanyia kama
mtoto wa kwanza.
Kaganda alisema baada ya matukio hayo,
mtuhumiwa aliendelea kujipumzisha nyumbani kwake, lakini ghafla
alivamiwa na kundi la wanakijiji waliopanga kumdhuru.
Hata hivyo, mtu huyo aliokolewa na askari
wa Kituo kidogo cha Polisi Igurubi, waliomchukua na kumpeleka Kituo
kikuu cha Polisi mjini Igunga.
Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Wilaya
ya Igunga, Mashaka Hilaly alithibitisha kuingiliwa kimwili kwa watoto
hao na kusema wameharibiwa vibaya katika sehemu zote za siri, hali
iliyolazimu kuwalaza hospitalini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni