Akitangaza
mpango huo mpya Dar es Salaam jana, Jaji Lubuva alisema Tume hiyo
itaanza maboresho ya daftari hilo kwa watu wote wenye sifa za kupiga
kura Septemba mwaka huu na kukamilisha kabla ya kura ya maoni ya Katiba
na Uchaguzi Mkuu 2015.
BVR ni mfumo wa kuchukua taarifa za mtu za kibaiolojia hasa alama za vidole.
Mwaka
2004, NEC ilianzisha Daftari la Kudumu la Wapigakura ikiwa ni pamoja na
ukusanyaji wa taarifa za wapigakura na uhifadhi wa taarifa za
kielektroniki.
Sanjari
na hilo, tume hiyo ilitoa vitambulisho vya wapigakura ambavyo pia
vimekuwa vikitumika kwa shughuli mbalimbali za utambulisho katika maeneo
kama benki, polisi, mahakamani, uhamiaji, ukataji leseni, usajili wa
simu na mengineyo.
Jaji
Lubuva alisema katika kazi hiyo ya uandikishaji, NEC imekusudia kutumia
Sh293 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa, mafunzo ya watendaji na
uandikishaji.
Maofisa
watakaotumika katika uandikishaji ni pamoja na waratibu wa uandikishaji
wa mkoa, maofisa waandikishaji ambao watakuwa ni wakurugenzi wa
halmashauri, maofisa wasaidizi watakaokuwa watatu kwa kila jimbo,
watendaji kata na waratibu wa elimu.
Mafunzo kwa watendaji hao yanatarajiwa kuanza Julai, 2014 na uandikishaji utaanza Septemba na katika vituo 40,015 kote nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni