Mchezaji wa Uruguay Luis Suarez atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa muda mrefu kucheza mechi zikiwemo za Kombe la dunia ikiwa atakutwa na hatia ya kumng’ata
mchezaji mwenzake wa Italia Giorgio Chiellini.
Shirikisho la soka duniani limeanzisha uchunguzi dhidi ya mchezaji huyo baada ya kuonekana akimng’ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao ya kombe la dunia.
Chiellini amedai Suarez amemng’ata katika bega lake la kushoto lakini Suarez amejitetea kuwa mchezaji huyo alijigonga kwake.
Refari wa mechi hiyo hakuchukua hatua yoyote dhidi ya Suarez.
Ikiwa atapatikana na hatia, Suarez huenda akazuiwa kucheza mechi 24 au kwa miaka miwili.
Suarez mwenyewe tayari amejitetea katika vyombo vya habari nchini Uruguay.
Suarez anasema Kuna mambo fulani ambayo hutokea uwanjani na hadhani ni vyema kuanza kuzua kashfa kutokana na mambo kama hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni