MSICHANA
Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo kata ya Vigwaza Wilayani
Bagamoyo mkoani Pwani yuko kwenye hali mbaya ya kiafya baada ya kuvimba
mguu na kuwa kwenye maumivu makali.Ugonjwa huo uvimbe huo ulianza kama
kipele kidogo miaka zaidi ya 10 iliyopita lakini kadiri siku
zilivyokuwa zikienda ndipo uvimbe huo ulizidi kuongezeka na kufikia
usawa wa mbavu.
Akizungumza
na waandishiw ahabari ambao walimtembelea nyumbani kwao alisema kuwa
uvimbe huo una ambatana na maumivu makali pamoja na homa kali hasa
nyakati za usiku.
“Niko
kwenye wakati mgumu kama mnavyoniona napata shida naomba nisaidiwe
kwani nimekwenda hospitali toka kipindi hicho lakini sikupata matibabu
zaidi ya kupewa vidonge tu ambavyo hupunguza maumivu lakini uvimbe uko
pale pale,” alisema Nata.
Nata
ambaye ana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (2) alisema kuwa
wakati tatizo hilo linaanza alikwenda hospitali mbalimbali lakini
hakuweza kupatiwa matibabu sahihi na kupelekea uvimbe huo kuongezeka
hadi hapo ulipofikia na kumkosesha raha.
“Naomba
wataalamu mbalimbali pamoja na wafadhili ili niweze kupata matibabu
sahihi ambayo yataondoa uvimbe huu ili name niweze kuishi kwa raha kama
wengine,” alisema Nata.
Kwa
upande wa baba yake Nata Mumbi alisema kuwa alimpeleka mwanae kwenye
hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu lakini hakuna mafanikio
yoyote.“Tatizo matibabu ambayo wanayompa si ya kina jambo ambalo
linasababisha mwanangu asipate nafuu, lakini kupitia vyombo vya habari
naomba wasamaria wema wamsaidie mwanangu ili aweze kupata matibabu
sahihi,” alisema Mumbi.
Aidha
alisema kuwa anashangaa kuona kila anapokwenda hospitali mwanae anapewa
vidonge tu jambo ambalo linafanya wakate tamaa ya kumpatia matibabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni