MCHUA
misuli wa Luis Suarez aliahirisha kwenda kupatiwa matibabu ya saratani
kuhakikisha mshambuliaji huyo wa Uruguay anakuwa fiti na kucheza dhidi
ya England.
Walter
Ferreira, mwenye umri wa miaka 63, alitarajiwa kwenda
kufanyiwa tiba hiyo kabla ya Kombe la Dunia. Faida ya uamuzi wake wa kuahirisha zoezi hilo ilionekana Alhamisi wakati mabao mawili ya Suarez yalipoitupa nje ya Kombe la Dunia England.
kufanyiwa tiba hiyo kabla ya Kombe la Dunia. Faida ya uamuzi wake wa kuahirisha zoezi hilo ilionekana Alhamisi wakati mabao mawili ya Suarez yalipoitupa nje ya Kombe la Dunia England.
Shukrani: Suarez akishangilia bao la kwanza na Walter Ferreira
Bao la kifo: Suarez akimtungua Joe Hart
Suarez,
ambaye alimkimbilia Ferreira baada ya kuifungia Uruguay bao la kwanza
la kuongoza, amekuwa akihudumiwa na mchua misuli huyo kwa wiki kadhaa
zilizopita.
Ferreira alisema: "Nawashukuru benchi la ufundi liliniamini na kunipa kazi ya kumhudumia Luis.’
Majukumu: Ferreira alisitisha kwenda kufanyiwa tiba ya saratani ili amhudumie Suarez
Suarez
alitoa shukrani zake kwa Ferreira kwa kumuwezesha kuwa fiti ndani ya
muda na kucheza dhidi ya England, ambao amewarudisha nyumbani mapema.
"Kuna mtu ambaye alijua kiasi gani nilihitaji msaada wake. Kama si yeye (Ferreira) hata hapa nisingekuwepo. Nililia sana na yeye,
kwa sababu ulikuwa wakati mgumu kiasi hicho, na wa kuchaganyanya kwa
sababu amejitoa mhanga kubaki na mimi kwa muda wote,"amesema Suarez.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni