Maajabu
yanaendelea duaniani, wiki hii tuliandika habari kutoka China iliyohusu
kijana aliyeng’olewa meno 132, lakini pia kuna habari nyingine kutoka
nchini humo ambayo imewaacha wengi midogo wazi.
Kwa mujibu wa
mtandao wa Shagalist, mwanaume aliyetajwa kwa jina la Mr. Chen,
mwanandoa mwenye umri wa miaka 44 na mkaazi wa Zhejiang, China
amegundulika kuwa alikuwa katika siku zake kama inavyokuwa kwa wanawake
kwa mzunguko wa hedhi(period) baada ya
kufika hospitali akilalamika sana kuwa na maumivu ya tumbo.
kufika hospitali akilalamika sana kuwa na maumivu ya tumbo.
Taarifa
zilizotolewa na madaktari wa hospitali ya Yongkang zinaeleza kuwa
mwanaume huyo alifanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa alikuwa na mfumo
wa uzazi wa mbegu za mwanamke ingawa alikuwa na uume.
Ingawa mwanamme
huyo aliwaeleza madatari kuwa amekuwa akishiriki na mkewe tendo la ndoa
kwa miaka kumi ya ndoa yao bila tatizo, madaktari hao waligundua kuwa
alikuwa anatoa mkojo wenye damu ambao uliwasababisha wafanye uchunguzi
wa kina na kugundua hali hiyo.
Msemaji wa
hospitali hiyo alieleza kuwa vipimo vya ACT Scan vilionesha wazi kuwa
alikuwa na uterus na ovaries (mayai ya uzazi), na kwamba madaktari
walieleza kuwa alikuwa amechelewa kupata matibabu kwa tatizo lake hilo
lisilo la kawaida.
Mr. Chen
mwenyewe alieleza kuwa alikuwa anasikia dalili ya vitu vingi visivyo
vya kawadia hata katika maumbile yake, na kibaya zaidi ni pale alipoanza
kuona anatoa damu badala ya haja ndogo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni