STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 12 Juni 2015

RASMI: MANCHESTER UNITED YAMSAINISHA MEMPHIS DEPAY

Klabu ya Manchester United imetangaza  rasmi kukamilisha usajili wa nyota wa kimataifa wa Uholanzi,  Memphis Depay na kumsainisha mkataba wa miaka minne.
Mpango wa kumsajili kinda huyu mwenye miaka 21 ulikamilika mwezi uliopita, lakini sasa dili limekamilika rasmi ambapo United imelipa ada ya uhamisho ya  paundi milioni 25.
Kiungo huyo anajiunga na Manchester United kutokea klabu ya PSV Einhoven ambapo alionesha kiwango cha juu kwenye ligi ya Uholanzi akifunga magoli 22 msimu uliopita.
Kijana huyo pia ameonesha kiwango kizuri timu ya taifa na wiki iliyopita alicheza mpira mwingi mno Uholanzi ikifungwa 4-3 na Marekani.
Memphis Depay anakuwa mchezaji wa kwanza  kusajiliwa rasmi na Man United majira haya ya kiangazi ambapo Louis van Gaal anatafuta wachezaji wa kuimarisha kikosi cha kushindania ubingwa msimu ujao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox