MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa hakuna uhasimu wowote kati yake na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Wawili hao wanahesabiwa kama wachezaji bora kabisa duniani kwasasa wakiwa wameshinda tuzo saba za Ballon d’Or zilizopita kati yao.
Ronaldo ambaye ndio alionyakuwa tuzo mbili za mwisho na kuwafanya wadau wa soka kudai kuwa mafanikio ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ndio yaliyomuhamasisha Messi naye kucheza kea kiwango cha juu msimu huu.
Hata hivyo, Messi amesisitiza kuwa haathiriki na kitu chochote ambacho Ronaldo anakifanya ndani na nje ya uwanja.
Messi amesema hakuna wala hakujawahi tokea uhasimu wowote kati yao kwani jambo hilo limetengenezwa na vyombo vya habari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni