Jose
Mourinho amesema kwamba, Eden Hazard lazima aongeze juhudi kurejesha
kiwango chake baada ya kushuhudia mabingwa hao wa EPL wakifumuliwa
magoli 2-1 nyumbani dhidi ya Crystal Palace wikendi iliyopita.
Magoli
ya Bakary Sako na Joel Ward yaliipa pointi zote tatu Palace wakati
Mourinho akisherehekea mchezo wake wa 100 akiwa nyumbani na kuwa kipigo
cha pili tangu Mreno juyo akabidhiwe majukumu ya kukinoa kikosi hicho
akiwa katika dimba la Stamford bridge.
Mourinho
amemgeukia Hazard ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa msmu wa EPL
msimu uliopita na wachezaji wengine baada ya timu hiyo kuwa na mwanzo
mbovu wa ligi, wakiwa na pointi nne ambazo wamezipata katika michezo
minne.
"Kama
wewe ni mchezaji bora katika ligi, nadhani itakuwa ni jambo jema kuwa
na kiwango ambacho kinafanana na msimu uliopita”, alisema.
"Sitaki
kuelezea kiwango cha mchezaji mmoja mmoja. Kwa ujumla, ni vigumu sana
kuwa ni kiwango kile kile endapo baadhi ya wachezaji hawachezi vizuri.
"Ukiwa una wachezaji sita au saba wanacheza vizuri halafu watatu au wanne hawachezi vizuri, ni vigumu sana kupata matokeo".
Aliongeza
kuwa anafanya kazi mchana na usiku kuhakikisha kuwa Chelsea inarejea
katika ubora wake katika wiki zijazo, lakini amesema itakuwa ni huzuni
kubwa endapo watabaki kuwa hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni