Manchester
City imetumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Etihad baada ya
kuwanyuka 3-0 mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini England, Chelsea
chini ya kocha wake, Jose Mourinho.
Sergio Aguero alianza kuifungia goli Man City dakika ya 31 akimalizia pasi safi ya Muivory Coast, Yaya Toure.
Nahodha wa City, Vicent Company alitia kambani bao la pili dakika ya 79 baada ya kazi nzuri ya David Silva.
Mbrazil, Fernandinho aliandika chuma cha tatu katika dakika ya 85 baada ya kusetiwa na David Silva.
TAKWIMU ZA MECHI
CHINI NI GOLI LA SERGIO AGUERO
CHINI NI GOLI LA VICENT COMPANY
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni