KLABU ya Chelsea imekubali kusajili beki wa kushoto wa kimataifa wa Ghana, Baba Rahman kutoka klabu ya Augsburg ya Ujerumani.
Mabingwa
hao wa Ligi Kuu ya England ambao leo wamefungwa mabao 3-0 Manchester
City, wamesema watamsainisha Mkataba wa miaka mitano nyota huyo wa Ghana
kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 14.
Katika
dili hilo, beki huyo atapewa Pauni Milioni 3.5 zaidi katika posho
kulingana na kiwango chake Chelsea, Pauni 700,000 baada ya mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 21 kufikisha mechi 20 na nyingine Pauni Milioni
3.5 atakapofikisha mechi 100 — maana yake thamani yake inaweza kufika
Pauni Milioni 22.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni