Moja ya wachezaji waliotikisa vicha vya habari za michezo
mwishoni mwa Juma lililopita ni Straika mpya wa Simba, Kelvin Ndayisenga, raia wa Burundi.
Nyota huyo alifunga goli lake la kwanza Jumamosi iliyopita Simba
ikishinda 2-1 dhidi ya URA ya Uganda katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Baada ya mafanikio hayo, Ndayisenga amesema anajiamini kuwa
atakuwa msaada mkubwa wa Wekundu wa Msimbazi ambao hawajawahi kutwaa ubingwa
tangu mwaka 2012, huku akikiri kuwa kikosi cha klabu yake mpya kina mpangilio
bora.
“Simba ni timu nzuri, ina mpangilio bora, nikibaki hapa
ninaamini nitafanya vizuri. Ninajiamini,
nitakuwa msaada mkubwa katika kikosi cha
Simba,” alisema Kelvin.
Kocha mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr amewapa
mapumziko ya siku kadhaa wachezaji wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni