Baada
ya kushinda 5-4 dhidi ya Sevilla na kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup
katika mechi ya fainali iliyopigwa nchini Georgia Jumanne iliyopita,
Barcelona walijikuta wakichezea kichapo cha 4-0 kutoka kwa Athletic
Bilbao kwenye mchezo wa kwanza ya Spanish Super Cup uliopigwa Ijumaa
iliyopita.
Barcelona wanahitaji ushindi wa magoli 5-0 ili kupindua matokeo hayo.
Mechi ya marudiano inapigwa usiku wa leo uwanja wa Camp Nou kuanzia majira ya saa 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Lionel Messi na Luis Suarez jana wamefanya mazoezi na wachezaji wenzao na bila shaka ndio wataongoza safu ya ushambuliaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni