Graeme
Souness amepinga mawazo ya mchambuzi mwenzake wa soka anayedai kwamba
kitendo cha John Terry kutolewa jana katika mechi dhidi ya Manchester
City ni kumtaarifa mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abromavic kuwa maisha ya
soka ya nahodha huyo yanaelekea ukingoni.
Kwa mara ya kwanza nafasi ya Terry ilichukuliwa na Kurt Zouma baada ya dakika 45 tu.
Haijawahi kutokea Kwa Terry kufanyiwa 'sub' katika mechi 177 chini ya kocha Jose Mourinho.
Akizungumza kwenye uchambuzi wa baada ya mechi wa Sky Sports, Souness, anaamini Terry alitolewa kwasababu tu ya presha ya Mourinho.
"Nadhani Terry alikuwa bora kuliko Gary Cahill, sikuona kama alicheza vibaya. John Terry ni kiongozi". Alisema Souness.
"Nadhani
kocha anajaribu kumwambia kwa vitendo mmiliki wa timu kwamba anahitaji
wachezaji zaidi. Kama stori ni za kweli basi anapenda wachezaji wengi
(Mourinho). Nadhani alikuwa anasisitiza hoja hiyo kwa vitendo akimtoa
Terry".
Souness alikuwa anabadilishana mawazo na mchambuzi mwenzake, Niall Quinn, ambaye alidai kwamba kitendo hicho ni dalili ya soka la nyota huyo wa zamani wa England kumalizika.
Quinn,
mchezaji wa zamani wa Manchester City anaamini sasa Terry anakabiliwa
na changamoto ya kupigania namba yake katika kikosi cha kwanza.
"Tuliona
picha zake akiwa kwenye benchi baada ya sub, naamini yeye mwenyewe
ameshaanza kuwaza kwamba anakwenda kugombania namba kwenye timu".
"Sidhani
kama Terry atacheza wikiendi ijayo (dhidi ya West Brom). Naamini ana
kazi kubwa ya kumshawishi kocha wake. Huu unaweza kuwa mwanzo wa kuisha
kwa soka lake".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni