Raheem Sterling tayari amezoea maisha ya Manchester City akitumia jezi yake mpya namba 7 katika uwanja wa Etihad.
Nyota
huyu aliyesajiliwa kutoka Liverpool kwa paundi milioni 49 ameanzisha
logo yake ya kibiashara kama alivyofanya Mwanasoka bora wa dunia,
Cristiano Ronaldo ambaye hutumia tag ya 'CR7'.
Baada
ya kupewa jezi namba 7, Raheem anavalia viatu vya rangi ya pink na
ameandika jina la mtoto wake wa kike , 'Melody Rose' pamoja na tag ya
'RS7'.
Logo hii inafanana na ya Ronaldo ambaye ameiendeleza na kuwa brand kubwa zaidi duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni