Mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga uliochezwa jumamosi ya tarehe 20 kwenye uwanja wa Taifa umeingiza kiasi cha shilingi milioni mia nne na tisini (Tsh. 490) kutokana na idadi ya mashabiki 54, 074 waliolipa tiketi kwenda kushuhudia mtanange huo.
Katika mchezo huo ambao mabingwa watetezi Yanga waliibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya mtani wao Simba waliomaliza pungufu katika mchezo huo. Katika huo mchezo kiingilio cha chini kilikuwa ni shilingi 7000 wakati kiingilio kikubwa ilikuwa ni shilingi 30000
Kiasi hicho cha pesa ni kikubwa kulinganisha na kile kilichopatikana kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ulifanyika katika huo huo Octoba 20 ambapo Yanga pia waliibuka na ushindi kama huu walioupata juzi.
Kutokana na hali hiyo timu hizo bado hazijaifikia rekodi walijiwekea ya kukusanya shilingi 500.7 milioni katika mchezo uliopigwa mwezi wa tano tarehe 20, 2013 mchezo ulioshudia sare ya magoli 3-3
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni