BUTOYI (KULIA) AKIMDHIBITI SSERUNKUMA KWENYE MICHUANO YA KAGAME JIJINI KIGALI, RWANDA. |
Beki Hassan Butoyi raia wa Burundi anatarajia kutua leo mjini Zanzibar
kuanza majaribio ya kutafuta nafasi Simba.
Butoyi anayekipiga katika kikosi cha Telecom ya Djibouti amekamilisha
mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.
Mazungumzo hayo yamefanyika mjini Kigali na sasa Butoyi anatua leo
Zanzibar ambako Simba imeweka kambi chini ya Kocha Patrick Phiri.
Hata hivyo Simba imeshakamilisha wachezaji watano wa kimataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni